KWA AJILI YA KUTANGAZA HARAKA
PIA INAPATIKANA KATIKA LUGHA ZA Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, Kireno, Kibahasa Kiindonesia
Mawasiliano:
Daliza Jimenez, SSF Hub, info@ssfhub.org
Jukwaa Jipya la Kimataifa Linalounganisha Wavuvi Wadogo ili Kuboresha Uendelevu na Riziki
Jukwaa tendanishi la lugha nyingi linawaleta pamoja wavuvi, wafanyakazi kwenye uvuvi, jumuiya na washirika
(WASHINGTON – Feb. 1, 2021) Muungano wa kimataifa wa washirika wanaofanya kazi katika na pamoja na wavuvi wadogo umezindua Kitovu cha Nyenzo na Ushirikiano cha Uvuvi Mdogo, au Kitovu cha SSF,jukwaa la mtandaoni ambalo ni tendanishi na lenye lugha nyingi kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa uvuvi mdogo na maendeleo ya jamii. Uzinduzi wa Kitovu cha SSF unafanyika sambamba na mkutano wa mwaka wa Kamati ya Uvuvi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo unaofanyika wiki hii, na unashughulikia Miongozo ya Hiari ya FAO kwa ajili ya Kuwa na Uvuvi Mdogo Endelevu katika Muktadha wa Usalama wa Chakula na Kuondoa Umasikini (au Miongozo ya SSF) ili kusaidia riziki za wavuvi wadogo na jumuiya za uvuvi.
"Uvuvi ni uti wa mgogo wa jamii za wavuvi waishio pwani na bara duniani kote, ukiwapa chakula na lishe, ukisaidia ajira zinazohusiana na uvuvi, husaidia kuondoa umasikini, hudumisha uhusiano wa kitamaduni na mifumo ya maji ya bahari na maji baridi, na kukiwa na ushawishi mkubwa kuhusu bioanuwai," alisema Dkt. Simon Cripps, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Marine Conservation for the Wildlife Conservation Society. "Kitovu cha SSF kitawaunganisha wavuvi na wadau wengine duniani kote ili kujifunza kutoka kwa kila mmoja, kushiriki taarifa na hatimaye kitaboresha maisha ya watu, matumizi endelevu ya bahari na maji baridi yenye ubora na uhifadhi wa viumbe asili vya bahari," aliongezea.
Sekta ya uvuvi mdogo hutoa michango mingi muhimu katika afya ya mifumo ya maji ya bahari na maji baridi, usalama wa chakula na lishe, riziki na kuondoa umasikini duniani kote. Kitovu cha SSF hutimiza hitaji muhimu la kuwasaidia wavuvi na jamii za uvuvi kushiriki visa na uzoefu wao pamoja na wenzao duniani kote na kupata teknolojia za kisasa kabisa na utafiti kuhusu tasnia ya uvuvi mdogo.
Wanajumuiya wa Kitovu cha SSF wanaweza kushiriki katika lugha 20, na wanaweza kushiriki katika majukwaa ya mijadala ya mtandaoni, makundi ya kieneo na yanayojikita katika mada maalumu, habari picha, nyenzo za kutumia ili kusaidia kufanya maamuzi katika eneo husika, video na visa vya mifano. Hii huwezesha jumuiya hii ya kimataifa ya uvuvi mdogo kuhusiana na kushirikiana kuliko hapo awali. Kitovu cha SSF ni rahisi kutumia, kinafikika kwa njia ya simu na kompyuta, pia kinajumuisha tafsiri za papo hapo ili jumuiya iwasiliane bila kikwazo cha lugha.
"Kuwa na uwezo wa kupata taarifa na uzoefu kutoka duniani kote huchangia kuwawezesha watendaji wa tasnia ya uvuvi mdogo, na kuwafanya washiriki kikamilifu au kuongza michakato ya kufanya maamuzi kuhusu riziki zao," alisema Vera Agostini, naibu mkurugenzi wa Kitengo cha Uvuvi katika shirika la FAO. "Pia huwezesha washirika wa maendeleo kujifunza kuhusu nyenzo za kila mmoja na uzoefu na kufungua fursa kwa ajili ya aina ya ushirika na ushirikiano ambao tutahitaji ili kutekeleza Miongozo ya SSF."
Uvuvi na vyakula vya majini ni muhimu sana katika kukidhi hitaji letu la kidunia kwa ajili ya lishe na riziki," alisema Jenny Oates, Meneja wa Kitengo cha Kukukuza Maarifa katika shirika la Blue Ventures. "Kazi tisa kati ya 10 za kudumu na za muda katika tasnia ya uvuvi zipo katika uvuvi mdogo, na karibu nusu ya nguvu kazi ni wanawake. Karibu samaki wote wanaokamatwa na wavuvu wadogo wanatumiwa sehemu husika. Wavuvi wadogo wanastahili kusaidiwa, na Kitovu cha SSF ni njia moja wapo ambayo inatumika kusaidiana."
"Ninashukuru sana kuwa na Kitovu hiki kwa sababu kimeweka mkazo zaidi kwenye SSF. Ni mara yangu ya kwanza kuiona [tovuti kama hii] iliyojikita zaidi kwenye jiamii ya wavuvi," alisema Mario Gasalatan, msadi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO) na mwakilishi wa wavuvi kutoka Jiji la Cebu, Ufilipino.
Kitovu cha SSF kiliandaliwa kwa ajili ya na pamoja na wavuvi, wafanyakazi kwenye uvuvi na jamii zao na washirika kupitia mchakato shirikishi, kwa lengo la kuwawezesha kushiriki maarifa na kujifunza kutoka kwa kila mmoja. Zaidi ya watu 100 kutoka katika nchi 19 tofauti, wakiwakilisha mashirika yao ya uvuvi, makundi ya hifadhi na washauri wataalamu, wametoa michango katika utengenezaji wa Kitovu hiki. Ushirikiano huu muhimu umesababisha uundwaji wa vipengele vya SSF kama vile majukwaa ambapo watumiaji wanaweza kuchangia mada wanazozipenda, kushiriki visa na kuuliza maswali. Wageni wanaotembelea tovuti hii (Kitovu) pia wanaweza kutumia maktaba ya nyenzo ikiwa na visa vya mfano, nyenzo za usimamizi, kozi za mtandaoni bila malipo na nyenzo nyingine kutoka FAO, NGO na mashirika mengine. Kitovu cha SSF kitaendelea kuboreshwa kwa kutumia teknolojia za kisasa za SSF, utafiti na mafanikio.
"Kupitia Kitovu hiki, jumuiya ya SSF inachukua hatua moja zaidi muhimu katika kuelekea kujenga uwezo duniani kote ili kusimamia biashara ya uvuvi kwa namna endelevu ili kwamba jamii zifanikiwe licha ya changamoto nyingi wanazoweza kukabiliana nazo, kuanzia mabadiliko ya hali ya hewa hadi COVID, na usalama wa chakula na lishe," alisema Eric Schwaab, makamu wa rais mwandamizi wa programu za Bahari na Mifomu ya Mazingira, EDF. "Kitovu cha SSF kimeundwa ili kuwapa wavuvi nyenzo wanazohitaji ili wafanikiwe dhidi ya changamoto hizi na nyinginezo."
Kitovu cha SSF kinaweza kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, ambayo yanajumuisha kukomesha umasikini, kuongeza usawa, kulinda sayari na kuhakikisha afya na ustawi. Biashara za uvuvi mdogo ni muhimu sana katika kufanikisha malengo mengi kati ya haya, ikiwa ni pamoja na kusaidia kuondoa umasikini, kuwepo na usalama wa chakula, kusaidia afya njema na lishe na kuleta usalama wa kiuchumi kwa mamilioni ya watu. Kutambua wajibu wa tasnia ya uvuvi mdogo katika kusaidia jumuiya zinazokua na katika kufanikisha SDG ni njia muhimu ya kuelekea kuwa na siku zijazo endelebu kwa wote.
###
Abalobi
ABALOBI ICT4FISHERIES ni shirika la kijamii la Kiafrika, linalojikita kwenye wavuvi linalovuka mipaka ya kimataifa. Njozi ya ABALOBI ni kutoa mchango kwenye jamii za uvuvi mdogo zilizo thabiti, zenye usawa na endelevu nchini Afrika Kusini na nje ya mikapaka yake, kupitia uendelezaji wa pamoja wa teknolojia. Mbinu yetu inajikita katika kufanikisha matokeo yanayoonekana, yakiongozwa na programu za simu, ambazo zinahusu upatikanaji wa chakula cha baharini, biashara za uvuvi zilizo katika maandishi, minyororo ya ugavi ambayo ni ya usawa na uwazi, uhusiano wa karibu wa jamii na ujasiriamali kama vitangulizi muhimu katika kutekeleza hatua za maboresho ya muda mrefu ya kiokolojia yanayohusiana na mabadiliko katika kuwa na uendelevu wa kiokolojia. Tufuate Twitter @abalobi_app au tembelea tovuti yetu abalobi.org
Blue Ventures
Blue Ventures hutengenza mbinu za kimabadiliko kwa ajili ya kuchochea na kudumisha uhifadhi wa bahari unaofanywa katika sehemu husika. Blue Ventures hufanya kazi katika pwani za kitropiki, katika maeneo ambapo bahari ni muhimu katika utamaduni na uchumi wa sehemu hiyo, na limezijatiti kulinda bioanuwai ya bahari kwa njia ambazo zinawanufaisha watu wa pwani. Mbinu za Blue Ventures hufanya jukumu muhimu katika kujenga tena uvuvi mdogo, kwa kutoa njia zenye ufanisi na zinazoweza kutumika tena kwa ajili ya kurejesha upotevu wa bioanuwai, zikiboresha usalama wa chakula na kujenga ustahimilivu wa kiokolojia na jamii katika mabadiliko ya hali ya hewa. Ungana nasi kwenye Twitter @BlueVentures
Conservation International
Conservation International inafanya kazi ili kulinda maslahi muhimu ambayo mazingira ya asili huwapatia watu. Kupitia sayansi, ushirikiano na kazi ya uwandani, Conservation International inaendesha uvumbuzi na uwekezaji katika masuluhisho yanayojikita katika mazingira ya asili katika mgogoro wa hali ya hewa, ikisaidia ulinzi wa viumbe muhimu, na kuendeleza maendeleo ya kiuchumi ambayo yamejikita katika uhifadhi wa mazingira ya asili. Conservation International inafanya kazi katika nchi 30 duniani kote, ikiwawezesha jamii katika viwango vyote ili kujenga sayari ambayo ni safi, yenye afya zaidi na endelevu zaidi. Ifuatilie kazi ya Conservation International kwenye Conservation Habari, Facebook, Twitter, Instagram na YouTube.
Environmental Defense Fund
Moja kati ya mashirika makuu ya kimataifa yasiyo ya kiserikiali, Environmental Defense Fund (edf.org) inatengeneza masuluhisho ya yanayoleta mabadiliko katika matatizo makubwa zaidi ya kimazingira. Ili kufanya hivyo, EFD inahusianisha sayansi, uchumi, sheria, na ushirikiano wa sekta binafsi ambao ni wa kibunifu. Likiwa na zaidi ya wanachama milioni 2.5 na ofisi nchini Marekani, China, Mexico, Indonesia na Umoja wa Ulaya, wanasanyasi, wachumi, wanasheria na wataalamu wa kutunga sera wa EDF wanafanya kazi katika nchi 28 ili kubadilisha masuluhisho yetu kuwa vitendo. Ungana nasi kwenye Twitter @EnvDefenseFund
Fauna & Flora International
FFI inalinda spishi zilizopo hatarini na mfumo za kiikolojia duniani kote, ikichagua masuluhisho ambayo ni endelevu, yanayojikita katika sayansi na kuzingatia mahitaji ya wanadamu. Likifanya kazi katika nchi zaidi ya 40 duniani kote, FFI linaokoa spishi ili zisitoweke na viumbe hai visiharibiwe, huku likiboresha maisha ya wenyeji wa sehemu hizo. Likiwa limeanzishwa mwaka 1903, FFI ni shirika la kimataifa la uhifadhi wa mazingira lililoanzishwa zamani na ni shirika la misaada lililosajiliwa. Pata maelezo zaidi kwenye tovuti yetu fauna-flora.org au jiunge nasi kwenye Twitter @faunafloraint
International Pole & Line Foundation
International Pole and Line Foundation (IPNLF) linahamasisha usimamizi endelevu wa uvuvi wa kuwajibika wa tuna kwa kutumia ndoana, na mshipi (kwa pamoja huitwa 'moja baada ya nyingine') huku pia ukitambua umuhimu wa kulinda uchumi wa watu wanaowasaidia. Kazi ya IPNLF ya kutengeneza, kusaidia na kuhamasisha uvuvi wa tuna kwa kutumia ndoana inashikamana kikamilifu na Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030. Tunaamini utawala wa kimataifa ambao ni wenye ufanisi na usawa ni muhimu katika kulinda na kuhifadhi bahari, na hili linapaswa kufanikiwa kwa kuhakikisha ushiriki wa jamii za wenyeji na wakazi wa pwani katika mchakato wa kufanya maamuzi.
Uendelevu wa mazingira katika uvuvi wa tuna unaweza kufanikiwa pia kwa kukomesha uvuvi kupita kiasi na desturi za uvivi ambazo ni za uharibifu ambazo zinasababisha uharibifu wa spishi, viumbe na mifumo ya kiikolojia ya bahari ambayo tayari ipo hatarini. Ikishirikiana na wanachama wake, IPNLF huonesha thamani ya tuna aliyekamatwa kwa kutumia ndoano kwa watumiaji, watunga sera na katika mnyororo mzima wa ugavi. IPNLF hufanya kazi katika sayansi, sera na sekta ya chakula cha baharini, kwa kutumia mbinu zenye ushahidi, zinazojikita kwenye masuluhisho kwa kutumia mwongozo wa kimkakati kutoka Bodi yetu ya Wadhamini na ushauri kutoka katika Kamati yetu ya Ushauri wa Kisayansi na Kiufundi (STAC) na Kundi la Ushauri wa Masoko (MAG).
Ocean Outcomes
Ocean Outcomes (O2) ni shirika la kimataifa linalofanya kazi na jamii za wenyeji, biashara za uvuvi na tasnia ya chakula cha baharini ili kuboresha uendelevu wa kimazingira, kijamii na kicuhumi kwa biashara za uvuvi. Miradi ya Ocean Outcomes inayojikita katika uboreshaji wa kisayansi hujumuisha tathmini, mchanganuo wa mnyororo wa ugavi, uhusikaji wa mnunuzi, programu za ufuatiliaji, miradi ya kuboresha biashara za uvuvi na wadau kushiriki. Kwa kuhifadhi na kulinda biashara ya uvuvi, Ocean Outcomes husaidia afya ya muda mrefu ya jamii ya wenyeji, minyororo ya ugavi wa chakula cha baharini na rasilimali za bahari ambazo sisi sote tunazitegemea. Pata maelezo zaidi kwenye oceanoutcomes.org
Oceana
Oceana ni shirika la utetezi la kimataifa kubwa zaidi ambalo limejitoa kikamilifu katika uhifadhi wa bahari. Oceana inajenga upya bahari kubwa na zanye bioanuwai kwa kutumia sera zinazojikita kwenye sayansi katika nchi nyingi ambazo zinadhibiti theluthi moja ya uvuvi wa samaki mwitu. Ikiwa na ushindi zaidi ya 225 ambao unasitisha uvuvi kupita kiasi, uharibifu wa viumbe, uchafuzi wa mazingira, na kuua spishi zilizo hatarini kama vile kasa na papa, kampeni za Oceana zinaleta matokeo. Bahari iliyohifadhiwa humaanisha kwamba watu bilioni 1 wanaweza kufurahia mlo wenye afya wa chakula cha baharini, kila siku, siku zote. Pamoja, tunaweza kuokoa bahari na kusaidia kuilisha dunia. Tembelea www.oceana.org ili upate maelezo zaidi.
Wildlife Conservation Society
Ikiwa na wafanyakazi zaidi ya 4,000, shirika la Wildlife Conservation Society, linafanya kazi karibu nchi 60, likilinda idadi yote inayojulikana ya zaidi ya spishi 100 zilizopo hatarini na maili za mraba milioni 3.6 katika mabara manne na bahari za ulimwengu. Programu ya baharini ya kimataifa ya WCS inaunda na kutekeleza masuluhisho ya kibunifu ya bahari, likiongoza miradi ya uhifadhi wa mazingira ya asili katika nchi 24 kwenye bahari zote 5 ikiwa na timu ya wataalamu wa baharini zaidi ya 400. Programu zetu katika ngome za bioanuwai za pwani huimarisha ulinzi wa bahari, huboresha usimamizi wa biashara ya uvuvi, na huhifadhi spishi muhimu za baharini. Tunajikita katika uvuvi endelevu, matumbawe, uundaji na usimamizi wa MPA, papa na taa na mamalia wa baharini.
World Wildlife Fund
WWF ni shirika huru la uhifadhi likiwa na wafuasi zaidi milioni 30 na mtandao wa kimataifa unaofanya kazi karibu nchi 100. Dira yetu ni kusitisha uharibifu wa mazingira ya asili ya sayari na kujenga siku zijazo ambazo watu wataishi na mazingira ya asili bila shida kwa kuhifadhi uanuwai wa kibilojia wa dunia, wakihakikisha kwamba matumizi ya raslimali za asili zinazoweza kutumika tena yanakuwa endelevu, na kuhamasisha upunguzaji wa uchafuzi wa hali ya hewa na matumizi ya kupoteza rasilimali. Tembelea panda.org/news ili upate habari za hivi karibuni na nyenzo za vyombo vya habari; tufuate kwenye Twitter @WWF_media

Hati ya nukuu: Kitovu cha SSF
Agatha Ogada, Mtaalamu wa Usadizi wa Mshirika wa Uvuvi, Kenya, Blue Ventures
"Changamoto zilizopo katika uvuvi mdogo na wale wanaoutegemea ni kubwa. Kupitia Kitovu cha SSF, wale wanaofanya kazi katika tasnia hii wanaweza kuhusiana, kubadilishana mafunzo na kuboresha utaratibu wa kufanya kazi. Kwa mfano, katika majadiliano na mtaalamu wa uvuvi mdogo huko Pasifiki, niliweza kuskia mawazo ambayo yanaweza kutumiwa ili kushughulikia matatizo tunayoyakabili nchini Kenya. Kitovu hiki kinatoa sehemu maalumu kwa ajili ya kujadili, kufurahia mafanikio na kuunda masuluhisho ya kiubunifu kwa ajili ya uvuvi mdogo."
Imani Fairweather Morrison, Afisa Programu, Uvuvi Mdogo wa Kimataifa, Oak Foundation
"Wavuvi wadogo wanaeleweka kwamba wanavutiwa na uendelevu wa maisha yao na jamii za pwani. Kitovu cha SSF kinaleta masuluhisho, yanayotolewa na washirika ambao ni NGO, kwa wavuvi duniani kote katika lugha nyingi na huwawezesha kutafuta na kutumia masuluhisho ambayo wanaona yanafaa zaidi mazingira yao. Tunaamini kwamba uhusikaji wa mvuvi katika muundo wake utapelekea nguvu na uwezo wa juu, kwa kuwawezesha wavuvi kushiriki katika usimamizi wa biashara ya uvuvi duniani kote."
John Tanzer, Kiongozi wa Shughuli za Baharini, World Wildlife Fund
Kukiwa na vitisho vingi kwa afya ya bahari na ustawi wa jumuiya ya baharini, tunapaswa kuwa na ufanisi zaidi kuhusu kutengeneza na kutekeleza masuluhisho yanayoongozwa na jamii. Kitovu cha SSF ni nyenzo yenye nguvu katika kuwezesha ushirikiano wa maarifa, kujenga uwezo na kuongeza ushawishi kwa wavuvi wadogo."
Miriam Bozzetto, Mtathmini wa Kampeni, Oceana Brazil
"Uvuvi mdogo ni muhimu kwa maisha ya maelfu ya raia wa Brazili. Ndicho chazo pekee cha mapato kwa familia ambazo kihistoria ziliishi kutokana na uvuvi wa kijadi. Ingawa Brazil haikuwa na takiwmu za biashara za uvuvi kwa zaidi ya mwongo mmoja, tunajua kwamba asilimia 70% ya samaki wa nchi hiyo wanatoka katika uvuvi mdogo. Ni muhimu kwamba serikali na mashirikia yasiyo ya serikali yanayofanya kazi katika eneo la uvuvi yaelewe umuhimu na uanuwai wa uvuvi mdogo ili kuhakikisha kwamba sera za umma zinatekelezwa ili kuhakikisha haki za wafanyakazi hawa, vilevile uendelevu wa shughuli hizi unaweza kuimarishwa."
Dr. Philippa Cohen, Kiongozi wa Programu ya Utafiti, Ustahimilivu wa Uvuvi Mdogo, WorldFish
"Uvuvi mdogo una sifa kuwa upo changamani na unabadilika. Badala ya kusema tu bila maarifa kwamba kuna mbinu moja inayowafaa watu wote katika kujumuisha wavuvi wadogo, au kudumisha mafao yanayotokana na SSF, kitovu hiki cha SSF ni cha thamani, ni mkusanyiko wa thamani wa nyenzo na maarifa ambayo yametengenezwa na wavuvi wadogo, katika maeneo tofuati, kwa ajili ya muktadha tofauti na kwa makusudi kadhaa."
Roy Bealey, Mkurugenzi wa Uvuvi, International Pole & Line Foundation
"Kwa zaidi ya mwongo mmoja unaokuja ni muhimu kwamba tunaunganika pamoja ili kuboresha afya ya bahari na kuhakikisha kwamba uvuvi mdogo unaweza kuendelea kwa namna endelevu ukitoa usaidizi muhimu katika jamii zinazotegemea uvuvi. Ushirikiano utakuwa muhimu wakati Kitovu cha SSF kinatoa nyenzo yenye nguvu na kwa wakati ili kutusaidia kufanikiwa pamoja."
Sophie Benbow, Mkuu wa Bahari, Fauna & Flora International
"FFI inasaidia jamii za uvuvi mdogo duniani kote ili kushiriki katika shughuli za uvuvi zinazojali bioanuwai. Kitovu cha SSF kinatoa fursa bora kabisa kwa wavuvi wenyewe kwa ajili ya kushirikiana na wanzao duniani kote, kujifunza na kushiriki uzoefu, na kuboresha mbinu zao na kuimaisha uendelevu."